Videos

Baba mzazi wa Bob Junior ala shavu kwenye label ya Warner Music Finland (ni mwanamuziki maarufu Finland)

Bahati mbaya Watanzania wengine hawafahamu kuwa baba yake mzazi na rais wa Masharobaro, Bob Junior ni mwanamuziki pia na sio mdogo, ni supastaa nchini Finland.

rummy

Baba yake anaitwa Rummy Nanji aka Mr. B na ni muimbaji mkuu wa bendi maarufu ya nchini Finland, Mighty 44.

Hivi karibuni bendi hiyo imepata shavu la kusainishwa na lebel ya Warner Music Finland (chini ya Warner Music Group).

482647_10151434149844962_1558856532_n

Mighty44

Kupitia Facebook, Bob Junior alimpongeza baba yake kwa kuandika:

Hongera sana my dad & all crew ya mighty 44 band…u did it guyz…das wats up hiyo ni big deal Warner Music?????????? ohhh…. am proud of u baba..in shaa allah kila la kheri wakilisha Tanzania, umenipa mzuka sana nami nije fanya makubwa katika muziki niwe zaidi yako…I love u dad…Rummy R. Nanji.

Hata hivyo Bongo5 ilitaka kufahamu kwanini baba yake Bob Junior ni mwanamuziki maarufu nchini Finland lakini watanzania wengi hawamfahamu.

http://www.youtube.com/watch?v=Zr1DdGZpyzc

“Well wabongo si unajua tena mtu akifanya kitu kizuri kwa nje tunakuwa kama tunampotezea hivi. Ni mwimbaji baba yangu miaka mingi tu sana ni miongoni kwa top artists in Finland,” ameiambia Bongo5.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents