Burudani

Babu Tale ajibu tuhuma ya kuwabania baadhi ya wasanii ili wasifanikiwe

Meneja wa Diamond na Tip Top Connection, Babu Tale amefunguka na kuzungumzia madai ya kuwa huwa anawabania baadhi ya wasanii wa nje ya management yake ili kuwapa nafasi wasanii wake.
babu-tale

Akizungumza katika kipindi cha The Playlist cha Times FM, Babu Tale amesema wale ambao wanasema kwamba wanabaniwa, wameshindwa kukiamini kile wanachokifanya ndio maana hawafanikiwi.

“Ukiwa na mentality kwamba Tale ndio anaendesha watu, mimi nilishawahi kukwambia piga ngoma hii,” Tale alimuuliza mtangazaji. “Mimi sina radio wala TV. Unajua kila mtu ana mtanzamo wake, Ni kweli kuna watu wanasema mimi nimetawala muziki ni kweli, kwa sababu ngoma za wasanii wangu nilizotoa hivi karibuni ni kali, mimi kila siku nawaza media inataka kulipa kupiga ngoma, media haiwezi kulipa ngoma mbaya, kwa hiyo mimi nafikiria kesho,”

“Sijawahi kuwasimamia Weusi, lakini wanafanya vizuri kwenye muziki, mimi simsimamii Ommy Dimpoz na anafanya vizuri, ana jiamini na anafanya kazi yake katika ubora. Wapo pia ambao mimi nawasimamia na hawafanyi vizuri, kwa sababu hawajiamini na hawafanyi kazi nzuri. Nipo kwenye team ambayo ina njaa na mimi mwenyewe nina njaa, sitaki kufanya kazi yangu tu ilimradi, wakati natoa nyimbo kama namtoa underground, hata kama natoa nyimbo ya Diamond naangaika kama natoa ya underground,” aliongeza Tale.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents