Siasa

Balozi Polepole kupelekwa darasani kwanza chuo cha Diplomasia, Rais Samia asema

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi Humphrey Polepole, atawekwa darasani kwanza katika Chuo cha Diplomasia na akimaliza watazungumza.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Machi 15, 2022, Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma, mara baada ya kumuapisha Polepole kuwa Balozi, pamoja na Mkuu wa mkoa wa Njombe, Waziri Kindamba aliowateua jana kushika nyadhifa hizo.

“Mh. Balozi najua baada ya hapa watakuweka darasani kwanza pale Chuo cha Diplomasia, utakapotoka pale kabla hujaenda Malawi nitakutana na wewe kwahiyo tutazungumza kwa urefu,” amesema Rais Samia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents