Habari

Balozi wa kinywaji cha Moët & Chandon atua Tanzania na ujumbe maalum

Kinywaji kipya cha kimetambulishwa leo jijini Dar es Salaam ambacho kimenadiwa kuwa ni Kinywaji kizuri, chenye rangi ya Njano na chenye radha mwanana.

Balozi wa kinywaji cha Moët & Chandon Pierre-Louis Araud akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutambulisha kinywaji cha Moet &Chandon hapa nchini.

Akizungumza wakati wa kutambulisha kinywaji hicho Balozi wa kinywaji cha Moët & Chandon Pierre-Louis Araud amesema kuwa ni kinywaji chenye uhai na ukarimu, kikiwa na rangi ya njano iliyong’arishwa na dhahabu na kinajitofautisha na vingine kwa ustadi na utajiri wake wa ladha.

Amesema kuwa “Urafiki, ushirikiano na ukarimu” ni kati ya maadili ya chapa ya Moët. Moët & Chandon inashiriki katika kuunganisha watu ulimwenguni kote na kujenga urafiki wa kudumu.

“Tunapofurahia uzinduzi wa Moët Nectar nchini Tanzania, pia tunataka kusheherekea watanzania kama marafiki wapya wa Moët na tunaendelea kuwapa moyo wale wote wanaopenda kufurahia maisha kushukuru kwa kila wakati na kusheherekea mafanikio kila yanapotokea..’

Balozi wa kinywaji cha Moët & Chandon, Pierre-Louis Araud akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutambulisha kinywaji cha Moet &Chandon hapa nchini.

Harufu ya Moët Nectar Impérial ina wingi wa matunda ya kitropiki kama mananasi na maembe, viungo vitamu vya mdalasini na vanila. Kikiwa mdomoni kina mchanganyiko wa ladha nzuri ya krimu na mazabibu.

Mchanganyiko wa kinywaji cha Moët Nectar Impérial unajengwa kwenye muundo wa zabibu ya aina mbali mbali ikiwemo wa aina ya Pinot Noir (asilimia 40 kwa 50), pia aina ya Meunier (30 kwa 40) na pia aina ya Chardonnay kwa asilimia (10 kwa 20). Matumizi ya asilimia 20 hadi 30 ya mvinyo ambayo imehifadhiwa kwa uangalifu yanakamilisha uundaji wa kinywaji hiki na kukiboresha zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents