Burudani

Barakah The Prince adai Ben Pol ametoa boko

Barakah The Prince hajaupenda wimbo mpya wa Ben Pol, ‘Tatu’.

Muimbaji huyo ambaye pia ni mmiliki wa lebo ya Bana Music Records, amedai alitengemea Ben Pol angetoa wimbo mkali kutokana na fujo za hivi karibuni alizozifanya muimbaji huyo kwenye mitandao ya kijamii.

“Tuache kama mimi na yeye ni marafiki, nimeongea kama shabiki na kwa sababu pia ujue kitu kama kile ujue Dozen kwa mtu kama Ben Pol karisk sana, halafu kuja anatoa nyimbo mbaya. Hapo mimi ndio nilishangaa,” Barakah amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Nilitegemea hii nyimbo itakuwa hatari. Yaani nilijua hii ngoma sijui itakuwaje kwa sababu unajua Ben Pol ni msanii mzuri,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents