Burudani

Wakazi na ndoto ya kucheza NBA

Msanii wa Hip Hop nchini, Wakazi amesema kabla ya kujitumbukiza katika muziki kwa asilimia zote alitamani siku moja kucheza Ligi ya Kikapu Nchini Marekani (NBA) wakati akisoma katika nchini humo.

Wakazi

Wakazi amesema alipofika Marekani alikuta wenye uwezo zaidi ndipo akajitumbukiza katika rap music kwa sababu vitu hivyo viwili kwa nchi kama Marekani vina uhusiano wa karibu.

“Kabla sijawa msanii wa Hip Hop nilikuwa mchezaji wa basketball na ni vitu ambavyo navifanya kwa passion kabisa lakini nimeshindwa kufanya basketball katika level ya juu kabisa kwa sababu wakati nipo college Marekani nilikutana na watu wanaofanya katika level ya juu na kupitiliza,” Wakazi ameimbia East Africa Radio.

“Kupata tu namba kwenye timu ya college halafu baadaye uwezo wakupata opportunity ya kuwa drafted kwenye NBA ni kitu kigumu sana si kirahisi, ndio maana passion yangu ikawa imeegemea zaidi kwenye muziki,” ameeleza.

Katika hatua nyingine wakazi amesema huu muziki wa Hip Hop ambao tunaufahamu umezaliwa Marekani, ni kwamba utamaduni wa Wamarekani Weusi wakati wanapoteza muda wao utawakuta wanacheza Basketball au wapo kwenye kona wana rap.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents