Habari

Mwili wa mzee Kinyasu wasafirishwa Mwanza

Mwili wa marehemu Mzee Francis Maige Kanyasu(86), umeagwa leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kusafirishwa na serikali kwenda kijijini kwao wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamaii , Jinsia , Wazee na Watoto, Marcel Katemba ameongoza shughuli ya kuaga mwili huo alisema .

“Nawapongeza Muhimbili kwa juhudi zenu ni kweli mlitaka kuokoa maisha ya mzee wetu, lakini kazi ya Mungu haina makosa. Sina budi kuwashukuru majirani zake na uongozi wa Serikali ya mtaa wa Malapa kwa kujitoa naomba mfanye hivyo hata kwa wazee wengine,” amesema Katemba.

Mzee Francis Maige Kanyasu alizaliwa 1931 na kufariki dunia Mei 29 , 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents