Burudani

Barnaba awaasa wasanii kutoichakachua Bongo Flava kwa kuiga wanaijeria

Barnaba amewashauri wasanii wenzake kutoiharibu Bongo Flava kwa kutaka kufanya muziki kama wa Nigeria.

barnaba11

Akiongea na E-News ya EATV, Barnaba alisema, “Wasanii wengi ukiwauliza wanakwambia wanaenda na wakati wanafanya muziki wa kibiashara mimimi sikubaliani na hilo suala, mimi nadhani biashara ipo pale pale, inategemea na uimbaji na unahama vipi,” amesema msanii huyo.

“Hautakiwi kuwa unahama unaimba muziki wa kukimbia kwakuwa watu wengine wamehama, unaweza ukajikuta unabugi, unatakiwa utwist kidogo namna ya uimbaji. Mfano kama Christian Bella, hajahama kwenye muziki wake wa bendi lakini ameitwist kidogo, muziki wake ni ule ule wa bendi lakini badala ya dakiki nane, sasa hivi wake una dakika 3 au 4, amechanganya kidogo na Bongo Flava.”

“Nawashauri wasanii wenzangu kusikiliza sana muziki tofauti tofauti hata miziki yetu ya zamani ambayo ilikuwa bora hadi leo. Unaweza ukachukua hata nyimbo hizo lakini ukaziboresha zaidi ukapata muziki mzuri. Ule muziki wa Nigeria wao wenyewe wanachukua asilimia nyingi huku kwetu lazima tuwe wabunifu wa muziki wetu.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents