Burudani

BBA The Chase: Watano waingia dangerzone wiki hii, Feza na Nando wako salama

Hii ni wiki ya nane ya reality show ya Big Brother ‘The Chase’ na dalili bado ni nzuri kwa washiriki wa Tanzania Nando pamoja na Feza Kessy ambao wiki hii wameponea kuingia katika nomination za kutoka hivyo wanauhakika wa kuimaliza wiki ya nane bila hofu ya kutupwa nje.

the chase

Baada ya nyumba zote mbili Ruby na Diamond kupigiana kura za kutoka mapema jana (July 15), na baadaye wakuu wa nyumba kupewa nafasi ya ku ‘save and replace’, Annabel mshiriki wa Kenya hakupata bahati ya kuokolewa na mkuu wake wa nyumba ya Diamond Bimp aliyeamua kuijokoa mwenyewe na nafasi yake kumuweka Bassey.

Wiki hii jumla ya washiriki walioingia dangerzone ni watano, upande wa Ruby ni Pokello (Zimbabwe) na Angelo (Afrika Kusini), na upande wa Diamond ni Annabel (Kenya), Bassey (Sierra Leone) na Dillish (Namibia).

Zimebaki siku arobaini tu kabla mmoja kati ya washiriki waliobaki atangazwe kuwa mmiliki halali wa $300,000 zawadi kutoka kwa biggie katika msimu wa 8 wa reality show ambayo inaendelea. Tanzania ndio nchi pekee ya Afrika mashariki ambayo mpaka sasa washiriki wake wote wawili bado wako mjengoni, tena bila kuwa kikaangoni kwa wiki hii. Baada ya Eviction ya wiki hii Jumapili (July 21) watabaki washiriki 12 ikiwajumuisha Nando na Feza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents