Habari

BBC kuhamishia kituo chake cha Radio ya Kiswahili Afrika Mashariki

Shirika la habari la kimataifa la Uingereza ‘BBC World service’ lina mpango wa kuhamishia kituo chake cha radio ya Kiswahili pamoja na kitengo cha uzalishaji wa maudhui ya mtandao wa BBC Swahili, Afrika mashariki.

BBC-World-Service

Mkurugenzi wa BBC Global News Peter Horrocks anatarajiwa kutembelea Nairobi kuja kutangaza mpango huo wa kuhamishia kituo hicho Afrika Mashariki, pamoja na uamuzi wa kuileta timu nzima ya BBC Swahili karibu zaidi na wasikilizaji wake wa Afrika Mashariki.

Horrocks alisema kila wiki kumekuwa na ongezeko la watu million 20 wanaosikiliza BBC Swahili na idadi ya watu wanaotembelea mtandao wa bbcswahili.com wamekuwa wakiongezeka mwaka hadi mwaka, hivyo kuhamishia timu ya BBC Swahili Afrika mashariki kutakidhi mahitaji ya watu hao.

“Every week, around 20 million people tune in to BBC Swahili radio. Amka na BBC and Dira ya Dunia are household names among millions of Kiswahili-speakers. Traffic to bbcswahili.com has grown more than threefold year on year – with majority of users coming to us via mobile phones. By relocating the BBC Swahili teams to East Africa, we will better meet the demands of these people who come to the BBC for the news and information they trust. We are confident that our audiences will be the winners of this change and investment in Africa.”

Baada ya kukamilika mpango huo utengenezaji wa vipindi vya Kiswahili vya ‘Amka na BBC’ utahamishiwa Dar es salaam, Tanzania, na kipindi cha mchana ‘Dira Ya Dunia’ kitakuwa kikiandaliwa Nairobi, Kenya. Na uandaaji wa habari za mtandao wa BBC utakuwa ukifanywa sehemu zote mbili Dar es salaam na Nairobi.

SOURCE:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents