FahamuHabari

Beki wa zamani wa Barcelona hatiani kufungwa miaka 12 jela kwa ubakaji

Mchezaji wa zamani wa Barcelona na Brazil Dani Alves amefikishwa mahakamani nchini Uhispania akituhumiwa kumbaka mwanamke katika klabu moja ya usiku.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40 amekuwa gerezani bila dhamana kwa zaidi ya mwaka mmoja tangu kisa hicho kinachodaiwa kutendeka mnamo Desemba 2022.

Bw Alves anaweza kufungwa jela miaka 12 iwapo atapatikana na hatia.Kwanza alikanusha kukutana na mshtaki wake, lakini baadaye alisema walifanya mapenzi kwa maelewano.

Kesi yake itakamilika Jumatano.Zaidi ya watu 30 akiwemo Dani Alves na mkewe aliyeachana naye wanatarajiwa kutoa ushahidi wao.

Mahakama ya Barcelona siku ya Jumatatu ilikataa ombi lake la kuahirisha kesi hiyo ili apewe muda zaidi wa kujiandaa – ikikataa madai yake kwamba alikabiliwa na kesi na vyombo vya habari.

Mshtaki wa Bw Alves alikuwa miongoni mwa waliotoa ushahidi siku ya kwanza ya kesi hiyo – akizungumza nyuma ya skrini ili kulinda utambulisho wake.

Anadai kuwa alimvuta kwenye choo katika sehemu ya VIP ya klabu ya usiku huko Barcelona, ​​na kisha kumlazimisha kufanya naye mapenzi.

Binamu wa mwanamke huyo na rafiki yake, ambao wote walikuwa naye usiku wa kudaiwa kushambuliwa, pia walitoa ushahidi wao siku ya Jumatatu. Walisema kwamba Bw Alves alikuwa amempapasa na kuwatania mapema jioni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents