Burudani

Belle 9 ahamishia rasmi makazi yake jijini Dar, azitaja sababu zilizomuhamisha kwao Morogoro

Wasanii wengi wa muziki waliopo Dar wametoka mikoani, na ukijaribu kuwauliza sababu za kuhamia Dar hata kama mikoa wanayotoka kuna studio nyingi za kurekodi pamoja na vituo vya radio, wengi wao hutoa sababu za kuja karibu na connection muhimu za media, studio, na wadau muhimu wa muziki.

Belle99

Upande wa Belle 9 sababu hizo hazikumshawishi kwa muda mrefu kwasababu alikuwa akija Dar kufanya kazi na kurudi kwao Morogoro, lakini sasa mwimbaji huyo wa ‘Shauri Zao’ amehamishia makazi yake rasmi jijini Dar es salaam.

“Nimeamua kuhamishia makazi Dar es salaam kwasababu nimeamua kubadilisha mfumo wangu wa kazi nilizokuwa nafanya mwanzo na sasa hivi” Belle 9 ameiambia Bongo5.

Sababu nyingine aliyoisema Belle 9 ni kuwa, amekuwa akipata malalamiko na maoni kutoka kwa wadau tofauti wakiwemo ma-promoter, watangazaji na wadau wengine ambao walikuwa wakipata shida kumpata pale anapohitajika kwa haraka.

Aliongeza kuwa kampuni yake mpya ni sababu nyingine ya kuhamia Dar.

“Sasa hivi kwa vile nimefungua kampuni yangu ya Vitamin Music ambayo ofisi zake ziko hapa hapa Dar na mimi ndio CEO, kwahiyo kama mwenye kampuni ya VM niko na business shares wenzangu wote tuko hapa Dar es salaam, kwahiyo niko Dar es salaam rasmi.” Alimaliza Belle 9.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents