Habari

Benki ya Dunia yapitisha mkopo wa Elimu kwa Tanzania

Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia imeidhinisha mkopo wa Dola milioni 500 ikiwa ni zaidi ya trilioni moja kwa Tanzania fedha ambazo zitasaidia kuinua sekta ya elimu nchini kwa kusaidia kuimarisha shule za serikali na kuanzisha mifumo imara kusaidia wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo katika mfumo rasmi.

Taarifa iliyoandikwa katika ukurasa wa Twitter wa Msemaji Mkuu wa Serikali imethibitisha kuwa Benki hiyo imefanya maamuzi hayo ikiwa na lengo la kuinua elimu nchini.

”Benki ya Dunia yafanya uamuzi wa kihistoria yaidhinisha mkopo wa Dola za Marekani 500m (Zaidi ya TZS trilioni 1); kuunga mkono juhudi za Rais katika kuendelea kuinua elimu nchini. Hii ni ARIDHIO muhimu kuanza nayo mwezi aliozaliwa Baba wa Taifa,” Imeandika

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents