Habari

Benki ya NMB ilivyonogesha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Simiyu

Benki ya NMB ilivyonogesha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Simiyu

Wakati Mkoa wa Simiyu ukiwa mwenyeji wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Kitaifa Machi , 2020, Benki ya NMB imenogesha maadhimisho hayo kwa kutoa msaada wenye thamani ya sh. Milioni 26.

Msaada huo ni pesa taslimu kiasi cha sh. Milioni tano pamoja na tisheti zenye thamani ya Sh. Milioni 21, ambapo umekabidhiwa na Meneje wa Beki hiyo Kanda ya Magharibi Sospeter Magesse.

Akipokea msaada huo Katibu Tawala wa Mkoa Jumanne Sagini, aliishukuru benki hiyo kwa msaada huo walioutoa ambao alieleza utasababisha maadhimisho hayo kupendeza.

Sagini alisema kuwa NMB imekuwa benki pekee na mdau mkubwa wa maendeleo katika Mkoa wa Simiyu, kwani kwa miaka miwili mfululuzo imekuwa ikidhamini maazimisho ya siku  ya wakulima kitaifa ambayo yamefanyika mkoani hapo.

Alisema kuwa Ofisi ya Mkoa inamshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, kwani kila wanapowasilisha maombi ya msaada wowote kwake amekuwa hasiti kusaidia.

 Tunajua NMB imeshiriki mambo mengi kwenye Mkoa wetu ya maendeleo, kwenye Nanenane ambayo mwaka huu inafanyikia hapa kwa mara ya tatu, NMB wamekuwa wakishiriki kudhamini kila mwaka,” alisema Sagini.

Aliongeza kuwa, maandalizi yote yamekamilika na mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan.

Kaba ya kukabidhi msaada huo, Meneja huyo wa Kanda wametoa tisheti 1800 ambazo zitavaliwa na washiriki wote wa maazimisho hayo pamoja na pesa sh. Milioni tano kwa ajili ya kusaidia kukamilisha maandalizi.

Magesse alisema kuwa benki hiyo itaendelea kuwa mshirika mkuu na mkubwa wa maendeleo katika mkoa wa Simiyu, huku akitumia nafasi hii kuwataka wanawake kuchangamkia fursa ya mikopo midogo inayotolewa na benki hiyo.

Picha 7443: Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi – Sospeter Magesse (kushoto), akimkabidhi tisheti 1800 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu – Jumanne Sagini kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.  

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents