Burudani

Bill Nas atemana na Rada Entertainment ya TID, ajiunga na label mpya ‘LFLG’

Mkali wa Ligi Ndogo, Bill Nas ameachana na management yake ya zamani Rada Entertainment ambayo inamilikiwa na TID na kujiunga na label mpya itwayo ‘LFLG’.
Bill Nas

Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Bill Nas amesema yeye na Rada kwa sasa wamebaki kama washikaji.

“Rada sijaondoka ila mkataka wangu mimi na Rada uliisha kwa sababu ulikuwa wa mwaka mmoja, tena uliisha muda mrefu toka mwaka jana mwezi wa 12. Kwa hiyo kwa sasa nipo kama familia tu na TID mimi ni kaka yangu, ni mtu ambaye ana mchango mkubwa kwenye sanaa yangu, kwa hiyo always tupo pamoja, lakini kibiashara nipo ndani ya label ya ‘LFLG’, hii ndio label ambayo nafanya nayo kazi, hata Chafu Pozi, audio na video nimeziandaa nikiwa kwenye label mpya,” alisema Nas.

Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo wake wa Chafu Pozi, amesema ana inaimani atafanya vizuri zaidi ndani ya label hiyo mpya kutokana na ushirikiano uliyopo ndani ya label hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents