Burudani

Collabo 10 za Bongo zilizotisha katika robo ya kwanza ya mwaka 2016

Tupo mwezi May na hiyo inamaanisha kuwa tumeianza robo ya pili ya mwaka 2016. Mengi mazuri yametokea kwenye muziki katika robo ya kwanza. Leo nataka nizitambue collabo 10 za wasanii wa Bongo zilizotisha zaidi katika kipindi hicho. Katika orodha hii, zipo pia nyimbo za wasanii wa Tanzania waliowashirikisha au kufanya na wasanii wa nje.

1. AY f/ Diamond Platnumz – Zigo Remix

Nina uhakika kuwa hata robo tatu zingine za mwaka 2016 zikimalizika, ni kazi mno kwa collabo nyingine itakayokuja kuizidi nguvu ‘Zigo Remix.’ Ni kwasababu ukubwa wa collabo hii hadi unawaogopesha wasanii wenyewe, kwamba itawachukua nguvu na muda kuivunja rekodi iliyoiweka. Zigo Remix imeweka rekodi nyingi ikiwa ni pamoja na kuvutia views milioni 5.9 hadi sasa tangu iwekwe kwenye Youtube January 22. Imeshika chati nyingi za ndani na nje na ni wimbo uliopata rotation kubwa sana kwenye redio. Ni collabo ya wasanii heavyweight ambayo kwa kiasi kikubwa inadhihirisha ukubwa wa wasanii wa Tanzania kimuziki barani Afrika.

2. Harmonize f/ Diamond Platnumz – Bado

Hakuna ubishi kuwa kwa sasa kila anachokishika Diamond hugeuka na kuwa dhahabu. Bado ni wimbo wa pili wa Harmonize kuutoa akiwa chini ya WCB baada ya Aiyola. Na hadi sasa Bado unakuwa wimbo mkubwa zaidi katika career yake. Zaidi ya kupata rotation kubwa kwenye TV na redio kuufanya kukaa kwenye katika top three ya nyimbo zinazochezwa zaidi Tanzania (kwa mujibu wa Copyright Music East Africa, CMEA), Bado imevutia views za kushangaza katika muda mfupi sana. Hadi sasa video yake imeangaliwa mara milioni 3.4 kwenye mtandao wa Youtube tangu uwekwe February 29. Inashangaza kwasababu umeizidi hata collabo ya Diamond na AKA ‘Make Me Sing’ licha ya kuwekwa wiki kadhaa kabla yake. Lakini pia Bado ni wimbo wenye hisia na uliondikwa kwa ustadi mkubwa.

3. Diamond & AKA – Make Me Sing

Utawala wa Diamond kwenye orodha hii unaendelea. Make Me Sing ni wimbo wa ushirikiano wa maheavyweight hawa walioziunganisha Tanzania na Afrika Kusini kimuziki. Kwa AKA yeye mwenyewe alikiri kuwa wimbo huu ulimfungulia milango zaidi kwa sauti yake kusikika katika nchi ambazo hakuwahi kusikika. Wimbo huu pia umefanikiwa kushika chati kwenye vituo vya redio na TV barani Afrika, lakini pia ukiwa na views za kutosha Youtube. Hadi sasa video yake imevutia views milioni 3.2 tangu iwekwe February 12.

4.Sauti Sol & Alikiba – Unconditionally Bae

Huu ni wimbo mwingine wa ushirikiano uliozikutanisha 255 na 254 kimuziki. Wimbo huu pia ni miongoni mwa nyimbo zinazopata airplay ya kutosha Tanzania kwa mujibu wa chati za CMEA. Video yake iliyofanyika Mombasa, Kenya na kuongozwa na Justin Campus, iliwekwa March 10 na hadi sasa ina views milioni 1.6.

5. Darassa f/ Rich Mavoko – Kama Utanipenda

Darassa anasifika kwa kutengeneza nyimbo tamu tangu aanze kufahamika. Wimbo huu umemrudisha vizuri si tu Darassa bali pia Rich Mavoko ambaye miaka ya hivi karibuni hajawika sana. Wimbo huu umekamilika kwa mambo mengi lakini beat na chorus yake vinaufanya kuwa na nguvu zaidi kwenye masikio ya wanaousikia. Na kwa Darassa, Kama Utanipenda unakuwa wimbo uliofanikiwa zaidi kiasi cha video yake kupata rotation ya kutosha Trace Urban.

6. Fid Q f/ Taz – Walk if Off

Fid anauelezea wimbo huu kama ‘feel good track.’ Ni wimbo tofauti kidogo na tulizomzoea huku pia ukiwa ndio wimbo alioufanyia uwekezaji mkubwa zaidi kuliko zote alizowahi kuzifanya. Kwa mara ya kwanza wimbo huu ulimpeleka SA kwenda kufanya kichupa kikali zaidi katika career yake.

7. Mzee Yusuf f/ Vanessa Mdee – Hewallah

https://www.youtube.com/watch?v=3PQRwC7w9fg

Namsifia Mzee Yusuf kwa jinsi anavyofikiria nje ya boksi na kufanya muziki nje ya comfort zone yake. Pamoja na kujichukulia sifa nyingi kwenye muziki wa taarab alikopewa ufalme, Yusuf anafahamika kwa kujichanganya vizuri na wasanii wa Bongo Flava. Harakati zake zilizalisha wimbo huu aliomshirikisha Vanessa Mdee. Ni wimbo mzuri, mkubwa na unaoonesha pia upande mwingine sauti ya Vee Money.


8.P The MC f/ Jux – Na Mimi

https://www.youtube.com/watch?v=35exc-_qZeo

Na Mimi ni wimbo ninaouweka kundi moja na ‘Kama Zamani’ ya Mwana FA aliowashirikisha Wana Njenje. Ni wimbo wa hip hop unaosikika live sana jambo linalonifanya nimpigie saluti Dully Sykes kwa upishi wake. P ni miongoni mwa rappers bora kuwahi kutokea na uandishi wake umejaa ufundi usio kifani. Kwenye wimbo huu analay low kidogo na kumweka Jux kunamfanya ajiongeze mashabiki hasa wa kike. Mwisho wa wimbo huu sauti ya Vanessa Mdee inasikika.


9. QS International Music Band – So Hard

Nina uhakika kuwa huu ni wimbo ambao watu wengi hawaufahamu kutokana na kutopewa nafasi na pengine huo ndio udhaifu mkubwa Qs International ambao hutumia fedha nyingi kwa wasanii wake lakini kufeli kwenye promotion. So Hard ni wimbo wa wasanii wa Qs International Band inayoongozwa na Q-Chief. Kwenye wimbo humu wapo wasanii wengine kama MB Dogg, Kadja na wengine. Ni wimbo mzuri wa mapenzi na wenye hisia sana.


10. Cjamoker f/ Wakazi P The Mc, Ibrah One The Incredible & ZAiiD – CJAMOKER

Unaweza ukawa hujausikia wimbo huu kwenye kituo chako pendwa cha redio, lakini hii ni moja ya collabo hatari za hip hop mwaka huu. Imewakutanisha rappers mahiri kwa uandishi wa mashairi na verse zao zimepakwa rangi na beat kali ya producer Cjamoker.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents