Burudani

Billboard na Twitter washirikiana kuanzisha Chart ya nyimbo zinazojadiliwa zaidi Twitter

Mtandao wa kijamii wa Twitter umeungana na Billboard kuanzisha chart za muziki ‘Billboard Twitter Real-Time Charts’ zitakazotokana na tweets za mamilioni ya watumiaji wa Twitter wanaotweet kuhusu muziki na wanamuziki kila siku.

billboard_twitter_logo_650

Alhamisi ya wiki hii makampuni hayo mawili yametangaza mpango wa kuanzisha chart hizo zinazotarajiwa kuanza mwezi May.

Chart hizo zitahusisha nyimbo zinazojadiliwa na kuwa shared zaidi katika twitter, na zitakuwa zinawekwa katika mtandao wa Billboard.com pamoja na akaunti ya Billboard katika mtandao wa kijamii wa Twitter, @billboard.

“Tunashirikiana na Billboard ili kutengeneza uwanja wa kufuatilia mazungumzo kuhusu muziki, hii inamaanisha wasanii wanaposhare nyimbo na kujichanganyanya na mashabiki wao kwenye twitter, nguvu wanayoitengeneza sasa itaonekana kwa mashabiki wao, wanamuziki wengine na watoa maamuzi wa kiwanda cha muziki.” Alisema Bob Moczydlowsky, mkuu wa kitengo cha muziki cha Twitter


SOURCE: BILLBOARD

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents