Burudani

Blac Chyna athibitisha kutoka kimapenzi na ‘kibenteni’

Tukijikumbusha kuhusiana na ngoma ya ‘Love doesn’t ask why ‘ ya Celion Dion iliyotoka mwaka 1993 ambayo inazungumzia mapenzi. Basi Blac Chyna atakuwa moja ya mwanadada ambaye yeye linapokuja suala la mapenzi hawezi vunga.


Kwa mujibu wa mtandao wa The Shade Room imeelezwa kuwa mrembo huyo amethibitisha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na rapper YBN Almighty Jay. Kabla ya kuwa na mahusiano na kijana huyo Chyna amewahi kuwa na mahusiano na rapper Mechine.


Alipoulizwa na mtandao wa The Shade Room kuhusu mahusiano yake na rapper huyo, basi Blac hakujivunga kusema kuwa wapo kwenye mahusiano ya mapenzi. Wawili hao walionekana kwa mara ya kwanza Jumatano ya wiki hii wakiwa katika ukaribu usio wa kawaida huku habari zisizo rasmi zikidai kuwa ni wapenzi.

Wiki kadhaa zimepita tokea mrembo huyo akubwe na balaa la kuvuja kwa mkanda wa ngono unaomuonyesha yeye aliwa na mwanume asiyejulikana wakivunja amri hiyo ya sita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents