Habari

Bobi wine ataja majina 30 ya walioshikiliwa katika nyumba za mateso Uganda, haki za binadamu zamgeukia waziri wa usalama naye awajibu

Bobi wine ataja majina 30 ya walioshikiliwa katika nyumba za mateso Uganda, haki za binadamu zamgeukia waziri wa usalama naye awajibu

Kamati ya bunge ya haki za bindamu imemtaka waziri wa usalama wa taifa nchini Uganda Jenerali Elly Tumwine kutoa maelezo kama nchini Uganda kuna nyumba za mateso zinazojulikana kama Safe House. Hii ni baada ya mbunge ambaye ni msanii Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine kuifahamisha kamati hiyo jinsi serikali inavyowatesa watu na zaidi wana siasa wa upande wa upinzani katika nyumba hizo.

Waziri huyo wa usalama Jenerali Elly Tumwine amekiri kuepo kwa nyumba hizo na kudai kuwa huwa zinazotumiwa kwa njia ya kiintelijensia, “Hata mimi mwenyewe siwezi kufahamu ni nyumba ngapi zinazotumiwa na vikosi vyote vya ujasusi nchini Uganda.

Nyumba za safe house zipo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa siri na hivyo haziwezi kufahamiki, zipo kwa ajili ya kupata maelezo ya kina, upelelezi haufanywi hadharani, upelelezi unafanywa kwa siri hivyo unawaita watu sehemu ya siri , na kuanza kufanya upelelezi zipo kwa kupata maelezo ya siri na maelezo ya faida, na huwa wanafahamishwa,”Tumwine alifafanua.

Lakini kwa nini Safe house zinatuhumiwa kutoa mateso makali kwa watuhumiwa?

Kwa mujibu wa BBC. Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine ambaye ni mbunge aliyepo kwenye kama kamati hiyo ya haki za binaddamu alihoji kwa nini nyumba hizo zinawalenga wafuasi wa upinzani? “Kwa nini wengi wanaokamatwa ni wafuasi wa wanasiasa wa upinzani, hao ndio wamelengwa na ndio wanapotea, wanateswa na kuuwawa?”Bobi Wine alihoji. Jenerali alipinga vikali shutuma hizo na kudai kuwa kama kuna mtu ana ushaidi wa kuwa nyumba hizo zinawatesa na kuuwa watu basi wanapaswa kutoa ushaidi lakini hakuna anayeweza kuwapeleka kuona nyumba hizo zilipo.

“Anayetoa tuhuma hizo sharti awe na ushaidi, kama kuna mtu yeyote amepotea, ameuwawa au kukamatwa kinyume cha sheria na kuteswa ana uhuru ya kwenda kuripoti kituo cha polisi,”Jenerali Tumwine alihoji. Kyagulanyi aliwasilisha majina 30 ya watu walioshikiliwa katika nyumba hizo katika kamati hiyo ya bunge. Waziri huyo alikataa ombi la wabunge la kutaka kutembelea sehemu hizo nyeti.

Spika wa bunge alitoa siku 14 za kufanyia uchunguzi juu ya malalamiko ya wananchi juu ya nyumba hizo za siri kutumika kutesa wananchi. Vikundi vya kutetea haki za binadamu siku za nyuma ziliwahi kuhoji serikali juu ya nyumba hizo za siri zinazowashikilia watuhumiwa.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents