Burudani

Bushoke aweka wazi kuwa wimbo wa ‘Mume Bwege’alipewa na mtu

Bushoke ni miongoni mwa waimbaji na watumbuizaji wazuri waliowahi kukamata chati nyingi za muziki miaka kadhaa iliyopita kupitia hits zake mbalimbali ikiwemo ‘Mume Bwege’.

bushoke

Kitu ambacho huenda mashabiki wengi walikuwa hawakifahamu ni historia ya wimbo huo ambao mpaka leo Bushoke akiuimba kwenye matamasha huwa unapata shangwe nyingi sana.

Bushoke amesema kuwa idea ya wimbo huo ilikuwa ni ya rafiki yake ambaye baada ya kuupenda alimuomba wabadilishane nyimbo.

“Asilimia 60 ya ile nyimbo sikuianzisha mimi, aliianzisha jamaa mmoja anaitwa Juma Silk (J Silk) ile nyimbo yenyewe ilikuwa inahusu mtoto, yenyewe ilikuwa na verse moja inayosema mimi mweusi mtoto katoka mwarabu, ilipoishia pale mimi nikaipenda ile nyimbo kwa hiyo nikaendelea na ile nyimbo, na J silk kuna nyimbo yangu na mimi nikampa”. Alisema Bushoke kupitia Planet Bongo ya EATV.

Mwimbaji huyo ambaye amepotea sana kwenye chati kutokana na ukimya wa muda mrefu, pia amesema anafurahi kuona muziki wa Bongo unazidi kupiga hatua.

“Mi nafurahia maendeleo, naona muziki unapiga hatua kwamba watu wanazidi kuutambua, na watu wengi sana hata kwa raia na viongozi, wanajua wapiganie wapi watu wanataka sana haki za wanamuziki, wanajua wanamuziki wawe vipi na pia teknolojia inazidi kuchange, kwa hiyo watu wanajitahidi kupigana na hilo lakini mi naona mpaka hapamulipo muziki uko sawa.” Alisema Bushoke.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents