Michezo

CAF yamteua mwamuzi wa Tanzania kuchezesha fainali za AFCON kwa wanawake

Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) limemteuwa mwamuzi wa kike kutoka Tanzania, Jonesia Rukyaa kuwa miongoni kati ya waamuzi 10 watakaochezesha fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake itakayofanyika nchini Cameroon.

caf

Baada ya uteuzi huo Rais wa shirikisho la soka Tanzasnia (TFF), Jamal Malinzi amesema, “Namtakia kila la kheri, naamini kwamba Jonesia atafanya vema. Nina uhakika kuwa hii ndio njia yake pekee ya kufanikiwa zaidi kwani ipo siku atateuliwa kuchezesha hata fainali za Kombe la Dunia.”

Waamuzi wengine walioteuliwa kuchezesha mashindano hayo ni pamoja na Salma Mukansanga (Rwanda), Lydia Tafesse (Ethiopia), Carolyne Wanjala (Kenya), Suan Ratunga (Burundi), Maria Packuita wa Mauritius, Gladys Lengwe (Zambia), Akhona Zennith Makalima (Afrika Kusini), Jeanne Ekoumou (Cameroon), Aissata Amegee (Togo) na Mary Njoroge kutoka Kenya.

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Novemba 19 na fainali kuchezeka Disemba 3 ya mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents