Burudani

Camp Mulla waandaliwa party ya BET nchini Marekani


Kundi la kwanza la Kenya kuwahi kutajwa kuwania tuzo za BET, Camp Mulla linatarajiwa kwenda Marekani wiki hii kuhudhuria party iliyoandaliwa kwaajili yao huko Santa Monica, siku chache kabla ya kufanyika kwa tuzo hizo.
Taio Tripper, Young Kass, K’Cous, Karun ana Mykie Tuchi watapongezwa kwenye ukumbi uitwao Zanzibar kesho (June 28).
Hafla hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano wa taasisi mbili zisizo za kiserikali za GoodMakers Films na Creative Visions Foundation.
Wasanii wakubwa duniani akiwemo K’Naan, Akon, John Legend, India Arie na will.i.am wamealikwa pia ambapo Camp Mulla wanatarajiwa kutoa ushirikiano wao katika kampeni yao utetezi wa watu wenye ulemavu wa ngozi, albino.
Kundi hilo lililohit na ngoma ‘Fresh All Day’ litakuwa sehemu ya kampeni iitwayo ‘We are one under the sun’, itakayoelekezwa zaidi katika nchi za Afrika Mashariki ambapo maalbino wamekuwa hatarini kuuawa kutokana na imani za kishirikina.
Maelezo yaliyoandikwa na Mkurugenzi mkuu wa GoodMakers Tilo Ponder yalisema, “Camp Mulla wataungana na wasanii wa kimataifa kuimba wimbo maalum uliotengenezwa kukuza uelewa juu ya suala hili.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents