Burudani

Cardi B azidi kuporomoka chati za Billboard

Rapper Cardi B anazidi kuporomoka katika chati kubwa za muziki duniani za Billboard Hot100, kutoka nafasi ya pili hadi ya tatu ambayo ilikuwa ikishikwa na Logic kupitia ngoma ya ‘1-800-273-8255’.

Cardi B ambaye alishusha katika chati hizo mama za muziki na Post Malone kutoka namba moja ambako alidumu kwa takribani wiki mbili mfululuzo ila kijana Post Malone kwa kushirikiana na 21 Savage, waliweza kumuondoa mrembo huyo wa Offset katika nafasi hiyo.

Kwa sasa nafasi ya pili katika chati za Billboard Hot 100 inashikwa na Camila Cabello kupitia ngoma yake ya ‘Havana’ aliyomshirikisha rapper Young Thug.

Hizi ndiyo orodha ya juu katika chati za Billboard:

1.Post Malone ft 21 Savage – Rockstar

2.Camila Cabello ft Young Thug – Havana

3. Cardi B – Bodak Yellow (Money Moves)

4. Logic ft Alessia Cara & Khalid – 1-800-273-8255

5.Imagine Dragons – Thunder

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents