Burudani

Cassim Mganga aeleza sababu za kuto-shoot video ya ‘I Love You’

Cassim Mganga aliyejipa aka ya ‘Tajiri wa mahaba’, wiki hii ameachia wimbo mpya ikiwa ni takribani mwaka mmoja toka alipoachia hit song yake ya mwisho ‘I Love you’ mwezi July, 2013. ‘I Love you’ ni miongoni mwa nyimbo zilizofanikiwa kupenya kwenye mioyo ya mashabiki wengi na kusambaa kila kona ya mitaa ya jiji la Dar na mikoani pia, lakini kuna kitu kilichomiss kwa wimbo huo kukosa video.

Cassim

Cassim ameelezea sababu za wimbo huo kutoufanyia video japo tayari walikuwa wameshaanza kufanya maandalizi ya kushoot mwaka jana.

“Tulilipa kabisa gharama za video na kila kitu, sitaki kutaja tulilipa kwenye kampuni gani lakini tulilipa kabisa,” Cassim Mganga ameiambia Magic FM alipofanya mahojiano na Dj Tass. “Mwisho wa siku tukawa tumefeli tumeona muda umeenda tunafanyaje, ebana saizi tena tukianza kurudi nyuma tuseme tunashoot ‘I Love U’, sawa sio mbaya lakini hebu tufunge ukurasa tuone tunaangalia ukurasa mwingine tunafanyaje, all in all lakini naona I Love U bado inanidai…siku yoyote mi naweza nikafanya kitu chochote.”

Cassim ameongeza kuwa wimbo wake mpya uliotoka wiki hii uitwao ‘Moto Moto’, tayari una video iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana, hivyo kwa sasa wanasubiri waone jinsi audio itakavyopokelewa kabla ya kuamua lini waachie video.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents