Habari

Chama kikuu cha upinzani DRC Congo MCL chatishia kufanya maandamano

Chama kikuu cha upinzani DRC Congo MCL chatishia kufanya maandamano

Chama kikuu cha upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kimetishia kufanya maandamano na pia kutishia kuupinga uchaguzi mkuu baada ya mahakama ya juu kabisa nchini humo kusema mgombea wa chama hana vigezo vya kugombea nafasi ya urais.

Kiongozi wa chama hicho Jean-Pierre Bemba aliondolewa kwenye orodha ya wagombea nafasi ya uraisi baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha na mahakama kukosa imani na upande wa ushahidi katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.

Baada ya kufanyika vikao vya ndani, chama hicho cha MCL kimetangaza rasmi kuwa kitatangaza baadaye tarehe rasmi ya maandamano hayo , kufuatia uamuzi wa mahakama ya katiba kuondoa jina la mgombea nafasi ya uraisi Jean-Pierre Bemba katika uchaguzi mkuu ujao nchini humo.

Kwa muujibu wa chama cha MCL kimeyachukulia maamuzi ya mahakama hiyo ya katiba kama ya hovyo na yanayoweza kuiingiza nchi hiyo katika machafuko.

Katika taarifa ya chama cha Bemba, kimekitupia mzigo wa lawama tume ya uchaguzi pamoja na mahakama nchini humo kwa kuwa imejaa siasa jambo ambalo serikali imelipinga kwa nguvu zote.

Miezi miine kabla ya uchaguzi huo, swali kubwa ni kuwa je chama cha MCL kitamuunga mkono mgombea mwingine kutoka kambi ya upinzani? Ambaye bado ana fursa ya kugombea nafasi hiyo au watabadili mwelekeo na kushughulika na mchakato mzima?

Inaarifiwa kuwa kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa nchini humo Jean Pierre Bemba yuko mjini Brussels , alirejea mjini Kinshasa mwezi huu, lakini kurejea kwake tena nchini humo kumeahirishwa.

Chanzo BBC

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents