HabariTechnology

Changamoto kuwa fursa, miaka 21 bila giza, bila tanesco (Video )

Kila binadamu angegeuza changamoto zake kama Mzee George Ulaya kuwa fursa, basi maisha yangekuwa mepesi sana.

Kutana na Mzee Ulaya miaka 55 ambaye alianza kutafuta nishati ya mwanga akiwa na umri wa miaka 7 ili aweze kusoma akiwa huko kijijni kwao.

Kwa sasa amekuwa mzalishaji mkubwa wa umeme wa upepo na maji Sumbawanga akisherekea miaka 21 bila Giza akitumia umeme wa maji huku akiwa na karakana kubwa ya kutengeneza mashine na kuziuza kwa Watanzani na wageni wa nje.

Kwa sasa anajenga nyumba yake ya ghorofa, ana gari mbili lakini pia ana ndoto yakuzalisha umeme wa maji kwaajili ya Wanasumbawanga wote.

Mpaka sasa tayari amefunga mashine hizo kubwa zakuzalisha umeme wa upepo na maji kampuni zaidi ya 20 pamoja na watu binafsi.

Related Articles

Back to top button