HabariMichezo

Conte ampigia simu Harry Kane baada ya kuiua City

Antonio Conte amempigia simu nyota wake, Harry Kane na kumpongeza Mshambuliaji huyo kwa kuwa Mfungaji Bora wa muda wote wa Tottenham kwa goli lake la ushindi 1-0 dhidi ya Manchester City.

”Unanifanya nijivunie,”- Conte amesikika kwenye simu aliyokuwa akiongea na Harry Kane.

Kocha huyo wa Tottenham alishindwa kuwasili uwanjani kutokana na kufanyiwa upasuaji nchini Itali na kikosi kuongozwa na kocha msaidizi, Cristian Stellini.

Bao la Kane kipindi cha kwanza lilimfanya nahodha huyo wa England kufikisha mabao 267 kwa Spurs, na kuvunja alama iliyowekwa na marehemu Jimmy Greaves.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents