COSOTA yasema katika wasanii kulipwa Serikali itachukua asilimia 30 na wasanii asilimia 70

Wengi wanafahamu kuwa Serikali iliwaambia Wasanii wa Tanzania wasubirie baadhi ya taratibu zikiwekwa sawa ili waanze kulipwa kutokana na kazi zao kutumika sehemu mbalimbali mfano kwenye TV, Radio na maeneo mengine yanayotumia muziki yakiwemo baa na sehemu z akuuza muziki sasa utaratibu upo hivi,

Kupitia taarifa ya Afisa TEHAMA Mwandamizi COSOTA Segenge James amesema kuwa: “Mgao wa pesa ni kwamba Msanii atapata asilimia 70 na COSOTA inapata asilimia 30, tutapokua tunakusanya hizi pesa hazitokuwa zinakwenda kwenye masurufu mengine Serikalini ndio maana imekua 70% tunawapa wao na 30% tunatumia sisi kwa matumizi ya kuturahisishia kufikia maeneo mbalimbali kuwakusanyia wao pesa wanayotakiwa kuipata”

“Wataingia kwenye www.hakimiliki.co.tz wataweka taarifa zao za biashara na kupata control number na kulipia leseni yake ya matumizi ya kazi za muziki, tumefanya kikao na kuwaelimisha Maafisa Utamaduni na Maafisa Biashara ili wawape elimu hiyo Wafanyabiashara ili kuondoa usumbufu na mlolongo usiohitajika”

 

Related Articles

Back to top button