Technology

Apple yazindua simu mpya IPhone 13 Pro na IPhone 13 Pro Max, uwezo wake hatari watangaza na bei zake (+ Video)

Kampuni ya simu ya Apple imezindua simu mpya za IPhone ambazo ni Iphone 13 Pro na iPhone Pro Max, simu zake mpya za kisasa zikija na jibu kwamba kufanikiwa kwa iPhone 12 Pro na Pro Max.

Tangazo hilo lilitolewa wakati wa hafla ya uzinduzi wa bidhaa ya Apple siku ya Jumanne, ambapo katika hafla hiyo walifanikiwa kuzindua iPhone 13 na iPhone 13 Mini ambapo bei zake zinatofautia zikianzia $999 – $1,099 yaani sawa na Tsh mil. 2.3 hadi mil 2.5.

Kitu cha tofauti katika simu hizo ni ikiwa kama nyongeza kubwa ni pamoja na kamera mpya tatu nyuma yenye uwezo wa 120Hz na maisha marefu ya betri yaani betri yake ikielezwa kudumu.

Bei za Simu hizo zitaanza kwa bei sawa na IPhone 12 Pro za mwaka jana, na iPhone 13 Pro ikianzia $ 1,699) sawa na Tsh Mil 3.9 na IPhone 13 Pro Max ikianzia na $ 1,849) sawa na Tsh mil. 4.3.

Kama kawaida kwa iPhones za kiwango cha Pro cha Apple, kamera ni moja wapo ya tofauti kati ya iPhone 13 Pro na mfano wa kawaida. Lakini simu utendaji wake wa kazi unaongezeka na hii ni kwa aina zote za bidhaa ambapo betri yake inaelezwa kudumu sana ingawa haijawekwa wazi inadumu kwa muda gani kwa sababu ya kutofautiana matumizi. lakini pia ukubwa memory Card ni 1-terabyte.

Wakieleza ukubwa wa kamera wamesema kuwa Iphone 13 ina lensi tatu na lensi kubwa ya simu ya milimita 77 ambayo hutoa ukuzaji wa picha (Zoom) ukiongezeka 3x kutoka iPhone 12.

Apple pia inasema iPhone 13 Pro na 13 Pro Max zina ubora katika kunasa picha  kwani kamera zao zinaweza kukuza kitu kwa umbali wa kuanzia sentimita 2.

iPhone 13 Pro ina skrini ya inchi 6.1, wakati iPhone 13 Pro Max ikiwa na skrini ya inchi 6.7. Lakini pia kwenye kamera wakiongeza kuwa ina uwezo wa ku shot movie kama inavyoonekana kwenye hii video fuatilia kwa makini uweze kufahamu zaidi.

https://www.instagram.com/p/CT1e8BdDKvV/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents