Burudani

Daddy Mashona baada ya kufanya vizuri na ‘Falling In Love’ akiwa Soprano, kuja na ‘Mkamilifu ‘

⁠⁠⁠Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Mbeya, Daddy Mashona baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Falling In Love’ akiwa amemshirikisha Soprano, anajipanga kuachia wimbo mpya wiki hii.

Rapa huyo ambaye pia ni mmiliki wa studio ya Final music iliyopo Kijitonyama jijini Dar as salaam, amesema wimbo huo mpya utatoka pamoja na video.

“Naachia wimbo mpya pamoja a video ambayo imetayarishwa na director Hypa Ibadah toka studio za Fx studio zilizopo jijini Mwanza. Hii ni baada ya miezi sita iliyopita kuachia wimbo wa Falling in love niliomshirikisha Soprano musiq. Wimbo wangu mpya ‘Mkamilifu’ ambao pia umetayarishwa na producer Teaz Villah ndani ya studio ya Final Music ni wimbo ambao utateka macho na masikio ya Watanzania wengi kutokana na ubora wa mashahiri yake na video,”

Pia rapa huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kuendelea kumsupport kazi za muziki wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents