Daktari wa MJ avamiwa

Daktari wa MJ avamiwa
Mwanasheria wa aliyekuwa daktari wa Michael Jackson amesema hospitali
ya daktari huyo ilipekuliwa na polisi maalum wanaoshughulika na madawa
ambao walikuwa wakitafuta ushahidi zaidi wa kosa la mauaji dhidi ya
daktari huyo

Mwanasheria huyo alisema polisi hao wa kitengo cha madawa ya kulevya
waliingia katika hospitali na kuondoa baadhi ya vitu katika hospitali
hiyo.

Msemaji wa Dr.Conrad Murray aliliambia shirika la utangazaji la BBC
kwamba walichofanya polisi ni uvamizi, "Upekuzi uliofanyika ulifanyika
kwa kushtukiza na kutushangaza, ulimshangaza hata mwanasheria wa
daktari."

Polisi walisema daktari huyo siyo ktuhumiwa kwa sababu alikuwa katika
jumba la Michael Jackson akijaribu kuustua moyo wa Michael wakati
mwanamuziki huyo alipoanguka kutokana na maradhi ya moyo.

Msemaji wa polisi hao Violet Szeleczky alisema upekuzi ulifanyika, lakini kiufundi haukuwa uvamizi wa polisi.

Mwanasheria wa Dr Murray aitwaye Edward Chernoff alithibitisha upekuzi huo wa polisi ulifanyika.

Alisema,"hati ya upekuzi inawaruhusu polisi kupekua na kuzuia kitu
chochote, ikiwa pamoja na nyaraka ambazo wanaamini wanaweza wakapata
ushahidi utakaowasaidia kuthibitisha mauaji ya Michael."

Awali Chernoff alisema mteja wake ambaye ni Dr Murray amekuwa
akiisaidia polisi kwa mambo ambayo wanamuuliza na tayari ameishahojiwa
mara mbili na polisi kuhusu kifo cha Michael Jackson.

Polisi wameishafanya upelelezi katika maeneo mbalimbali kuhusu kifo cha
Michael na hivi sasa wanakusanya na kutafuta taarifa za rekodi za
madawa ukiacha rekodi ya madawa ambayo aliitoa Dr.Murray.

"Dr.Murray alikuwa daktari wa mwisho kumsaidia Michael Jackson kabla
hajafariki, lakini inaoneka tuhuma zote anapewa Dr.Murray," alisema
Chernoff.

Chernoff alisema anachukizwa na taarifa mbalimbali mbaya zinazotolewa
na vyombo vya habari dhidi yake ambapo inambidi atembee na walinzi saa
24.

"Hivi sasa hawezi kufanya kazi zake za udaktari, hawezi kwenda kazini
kwa sababu anasumbuliwa kila anapokwenda,"alisema Chernoff.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents