AfyaHabari

Dawa za mafua, homa zakwisha madukani Corona yashika kasi Beijing

Visa vya maambukizi ya Uviko vinaongezeka kwa kasi katika mji mkuu wa China Beijing, wakati nchi hiyo ikitafakari namna ya kuachana haraka na mkakati wake wa kuzia maambukizi ya ugonjwa huo.

Mamlaka za mji wa Beijingi zimesema kuwa watu 22,000 walifika hospitalini jana kuhusiana na maradhi hayo, ikiwa mara 16 zaidi ya idadi ya wiki moja iliyopita.

Leo hii China imesajili visa vipya 8,626 vya maambukizi, lakini idadi halisi inaweza kuwa ya juu zaidi kwa sababu wakati huu sheria inayowalazimu watu kuchukuliwa vipimo imeondolewa.

Dawa za mafua na homa zimenunuliwa na kwisha kabisa katika maduka ya dawa mjini Beijing, na uhaba wa vifaa vya kujipima unatarajiwa wakati watu wakivinunua kwa wingi kwa hofu kuwa maambukizi yatakithiri na kuathiri zaidi maisha ya mamilioni ya wazee ambao bado hawajapata chanjo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents