Burudani

Daz Baba ni mgodi uliotelekezwa na madini yake

Kizuri hakidumu. Miaka ya 2000 nilianza kumfahamu msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Daz Baba aliyekuwa ndani ya kundi la Daz Nundaz lililokuwa na wasanii watano ambalo lilifanikiwa kukiki na nyimbo kibao.

Daz-Baba11

Ndani ya kundi hilo Daz Baba ndiye alikuwa ni mkali zaidi kwenye uandishi wa mashairi ya kundi hilo, alifanikiwa kuongoza kwenye uandishi wa nyimbo kibao kama ‘Kamanda’ na ‘Barua’ ni nyimbo ambazo zimeendelea kuishi kwa miaka mingi bila ya kupotea tofauti na nyimbo nyingine za sasa zilizogeuka kuwa big G.

Nasikitika sana ninapomuona Daz Baba amepotea na mashairi yake wakati muda haujafika huku tasnia ilikuwa bado inamhitaji. Japo amesahaulika kutokana na maisha yake ya sasa lakini mashairi yake aliyowahi kuyaandika yatazidi kupenya kwenye masikio yetu.

Naikumbuka nyimbo yake ya ‘Elimu Dunia’ ni moja kati ya nyimbo ambazo wazazi na walimu wanaweza kuwatia moyo wanafunzi kupitia nyimbo ile kutokana na mashairi yake yenye uwezo wa kuishi miaka mingi.

Uwezo wake wa kuandika mashairi mazito ulimpatia jina jingine la Daz Mwalimu. Hakika alistahili kuongezewa jina hilo kwa kuwa alikuwa ni kama mwalimu kutokana na ujumbe unaoishi wa nyimbo zake kwa jamii iliyomzunguka japo wanasema mganga huwa hajigangi.

Natamani nimuone tena Daz Mwalimu anasimama na kurudisha heshima yake iliyopotea kwa miaka mingi ingawa hiyo ni ngumu kutokana na mchezo ulivyobadilika kwa sasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents