Burudani

Deal ya Sony Music kumzuia Davido kufanya collabo na Joh Makini na Alikiba?

Wiki iliyopita, Davido alikuwa msanii wa kwanza wa Afrika kuwahi kusaini mkataba wa dunia na label kubwa ya Marekani, Sony Music Entertainment.

12558854_881518835295729_129345812_n

Mkataba huo wa mamilioni ya dola, unamweka msanii huyo wa Nigeria kwenye nafasi nzuri ya kukuza jina lake duniani kote. Kwa sasa akiwa chini ya usimamizi wa label hiyo kubwa, kuna uwezekano mkubwa wa mipango yake mingi ya awali kuvunjika zikiwemo collabo alizokuwa amepanga kufanya.

Kama mambo yakiwe hivyo, wasanii watakaoathirika na hatua hiyo ni Joh Makini na Alikiba. Ni Davido mwenyewe ndiye aliyetangaza collabo na mastaa hao mwaka uliopita.

davido-Joh

Lakini kwakuwa sasa ameingia kwenye mikono ya watu wengine, huenda collabo hizo zikawa zimeyeyuka.

Ujumbe huu aliopost kwenye Instagram, unaonesha kila dalili kuwa kwa sasa Davido ana mabosi wapya na mipango mipya.

“On the phone with my new Bosses they say I have 2 weeks to have fun then it’s straight to work… They say it ain’t gon be easy but I know my God will pull me through,” aliandika.

Hata hivyo staa huyo ametumia weekend hii kusherehekea mafanikio hayo na mpenzi wake, Sira Kante.

12523519_1522587184711723_410106028_n

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents