Michezo

Dembele, Umtiti na Griezmann waiangamiza Italia (+video)

Jana usiku timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Ufaransa imeichakaza Italia goli 3-1 kwenye mchezo wa kirafiki wa FIFA.

Magoli ya Ufaransa yamefungwa na wachezaji wawili wa Barcelona Ousman Dembele na Samuel Umtiti huku goli la tatu likifungwa na mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann.

Goli pekee la Italia limefungawa na Leonardo Bonucci kunako dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Italia ambayo kwa miaka mitatu sasa inaonekana kupungua makali yake kwenye mchezo wa soka, mwaka huu pia haitashiriki kombe la dunia baada ya kushindwa kufuzu. Tazama magoli hapa chini ya mchezo huo

https://youtu.be/qOKfcl7ijUs

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents