Habari

Deni la Serikali ni TRIL 82.25 – CAG Kichere

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere, leo amewasilisha ripoti kuu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu Chamwino Dodoma ambapo moja ya aliyoyazungumzia ni deni la Taifa. “Kufikia June 30,2023 deni la Serikali lilikuwa Tsh. trilioni 82.25 sawa na ongezeko la 15% kutoka Tsh.trilioni 71.31 kwa mwaka 2021/2022, deni hilo linajumuisha deni la ndani Tsh. trilioni 28.92 na deni la nje Tsh. trilioni 53.32 kipimo kinaonesha deni hili ni himilivu” “Uwiano wa kulipa madeni na mauzo ya nje ni 12.7% chini kidogo ya kiwango cha ukomo cha 15% na uwiano wa malipo ya madeni na mapato ni 14.3% chini kidogo ya kiwango cha ukomo elekezi cha 18%” ——— Kichere.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B,.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents