Habari

Mashirika 8 yalikusanya Bil 23.7 nje ya GePG

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere leo amewasilisha Ripoti kuu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Chamwino Dodoma ambapo moja ya aliyoyasema kwenye ripoti hiyo ni kuhusu Mashirika nane kukusanya pesa nje ya mfumo wa malipo ya Serikali. “Nilibaini kuwa Mashirika 8 ya Umma yalikusanya mapato ya Tsh. bilioni 23.27 nje ya mfumo wa kielektroniki wa malipo ya Serikali (GePG) kinyume na waraka wa hazina namba 3 wa mwaka 2017, kushindwa kukusanya mapato kupitia GePG kunaweza kusababisha upotevu wa mapato na kufifisha juhudi za udhibiti na uwazi katika mapato ya Serikali” ——— Kichere.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents