Habari

Zilibadilishwa Mita 108088 kabla ya Muda

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere leo amewasilisha Ripoti kuu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Chamwino Dodoma ambapo moja ya aliyoyasema kwenye ripoti hiyo ni kuhusu mita za umeme zilizobadilishwa na TANESCO kabla ya muda wake. “Mita 10,8088 za umeme za TANESCO kati ya mita 60,2269 zilibadilishwa na TANESCO kabla ya kipindi cha uhai wa matumizi yake kuisha, kati ya mita hizo mita 13,493 zilibadilishwa ndani ya mwaka mmoja baada ya kufungwa kwake na mita 90,595 zilikuwa na muda mfupi wa matumizi kati ya mwaka mmoja na miaka 15 kinyume na muda unaokubalika kwa miaka 20 kwa mujibu wa TANESCO wenyewe” “Kubadilisha mita mapema kunasababisha gharama kubwa kwa TANESCO napendekez Wizara ya Nishati ichunguze sababu ya TANESCO kubadilisha mita mapema pia Wizara ihakikishe vipimo vya ubora wa mita vinafanyika ili kuongeza ufanisi wa mita” ——— CAG Kichere.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents