Habari

Bil 6. Zilizokusanywa hazikufika Benki – CAG Kichere

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere leo amewasilisha Ripoti kuu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Chamwino Dodoma ambapo moja ya aliyoyasema kwenye ripoti hiyo ni kuhusu Bilioni 6 ambazo zilikusanywa na Halmashauri lakini hazikuwasilishwa Benki. “Ukaguzi umebaini kuwa Halmashauri hazikukusanya Tsh. bilioni 61.15 kutoka katika vyanzo muhimu na vikubwa wakati Tsh. bilioni 6.19 zilizokusanywa hazikuwasilishwa Benki” “Hali hii inaathiri uwezo wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza miradi ya maendeleo na kutoa huduma bora kwa Jamii” amesema CAG Kichere.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents