Burudani

Diamond aeleza kwanini ‘alidedicate’ tuzo zake za Afrimma kwa Tiffah

Diamond amesema alikuwa na ndoto siku moja akipata tuzo ya mafanikio ya kazi zake aielekeze kwa mtoto wake, Latiffah.

diamond na Tiffah

Muimbaji huyo aliyeshinda tuzo tatu za Afrimma Jumapili hii ameiambia ya XXL ya Clouds FM kuwa amefanya hivyo kwa sababu mafanikio yake yanachangiwa na mtoto wake huyo.

“Unajua ilikuwa ni moja ya ndoto zangu, kwamba hiyo siku nikipata tuzo halafu nina mtoto na nikaidedicate hiyo tuzo kwa mwanangu. Inaleta picha nzuri sana na ukizingatia najitahidi kufanya kazi kwa umakini ili kesho na kesho kutwa mwanangu amezaliwa baba yake nikiwa fulani halafu akue anikute nimefulia kweli? Itakuwa hata kumtazama naona aibu. Napenda mwanangu anikute wakati Diamond yupo kwenye ukubwa wake,” alisisitiza Diamond.

Aliongeza, “amekuwa akinipa changamoto sana, kama kuimba niimbe sana, kutunga nitunge sana, kama kujituma nijitume sana. Kwahiyo nakuwa namuwaza kwenye kichwa ndio maana nikasema nimdedicate hii tuzo kwake. Unajua zamani nilikuwa nikisikia wazazi wanapenda watoto wao naona sometimes ni maneno yao tu. Lakini sasa hivi nafeel kabisa upendo yaani hata mtu akiweka picha mbili akinidiss mimi akamsifia mwanangu hainiumi sana kama kanidiss naona bora alivyomsifia mwanangu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents