Burudani

Diamond atoa kauli kufungiwa kwa wimbo Mwanza ‘show yangu moja ya nje nachangia serikali tsh milioni 48’

Rais wa WCB, Diamond Platnumz amekubali wimbo Mwanza alioshirikishwa na Rayvanny usipigwe redio na kwenye runinga kama taarifa ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) ilivyodai kwa kuwa wimbo huo hauendani na maadili ya Watanzania.

Katika taarifa hiyo aliyoitoa Diamond kupitia instagram, amependekeza wimbo huo usiondolewe YouTube kwa kuwa watoto hawaingii mitandaoni. Pia muimbaji huyo amedai wimbo huo uwenda ukawa ni kwaajili ya kimataifa ambapo amedai kwa show moja ya kimaifa analipa kodi ya tsh milioni 48.

Part 1:-
KWA WAZEE WANGU WA BALAZA LA SANAA TANZANIA (BASATA)
Kwanza kabisa niwapongeze kwa kazi nzito na nzuri Mnayoifanya….lakini pia niwape pole kwa changamoto mbalimbali mnazokutana nazo, maana najua ugumu mnaopitia katika kusimamia sanaa yetu Nchini…..Ujumbe wenu kuhusu Kufungiwa wimbo wa #Mwanza almaarufu kama #NYEGEZI wakuu nimeupata ila tu kwabahati mbaya mtoto wenu niko Canada katika harakati za kutafta rizki ili kuendelea kulijenga taifa na kuendelea kutangaza sanaa zetu, ila laiti ningelikuwa nchini ningekujamara moja kama mnavyonijuaga pindi mniitapo basi hufika haraka bila ukaidi…..
Tuki wama Wasani ambao tumesajiliwa tuna kila haki ya kuheshimu na kutii balaza letu la sanaa BASATA pindi linapotoa tamko…..kwasababu wao ndio wazazi na walezi wetu kwenye hii sanaa….na kwakutambua kuwa Sanaa ni kazi ya Ubunifu, na kwenye kubuni wakati mwingine kuna kuwa na usawa na wakati mwingine kutokuwa sawa ndiomaana mliteuliwa Nyinyi wazee wetu maalum kwa jili ya kuhakikisha wasanii wanapotoka nje ya Mstari mnawarudisha ili tuwe na sanaa ilio bora, tuzidi kufanikiwa, na kukua vyema na hata wasanii, mashabiki pamoja na taifa kwa ujumla lijivunie na linufaike na sanaa…..
ila Kwenye UFUNGIWAJI huu nami nilikuwa nina OMBI ama PENDEKEZO kwa balaza letu pendwa la sanaa Tanzania (BASATA)….
Licha ya kuwa ni kweli #NYEGEZI ni eneo na kituo cha Mabasi kilichopo MWANZA, lakini pia ni vyema Kama balaza letu pendwa la sanaa kutambua pia kuwa sio kila Nyimbo ni kwajili ya watoto wadogo….Hivyo kusema isipigwe kwenye TV na Radio tumekubali, lakini iwe Kwenye Ule muda ambao serikali uliuweka wa kuwa watoto wako macho, ila pale wanapolala, basi uruhusiwe ili walengwa wautazame…. PILI:- kusema tuifute Mitandaoni pia, naomba pia Balaza letu pendwa litutazame pia na hapo…. kwasababu mtoto mdogo tunaemlenga kumlinda asiharibikiwe kimaadili hapa, sizani kama mzazi wake anaweza kumruhusu akaperuziperuzi bila mipaka mitandaoni maana kama kweli ana uwezo wa kufanya hivyo basi anauwezo wa kwenda kuangalia hata Video za utupu, na vitu vingine ambayo wote tunafahamu ndio hatari na Madhara zaidi kwa watoto, kuliko hichi kinyimbo chetu cha #MWANZA NYEGEZI

PART 2:- TATU:- Wazee wetu, vijana wenu ama wasanii wenu sasahivi tumefanikiwa kuingia kwenye masoko mbalimbali hivyo sio kila nyimbo ni kwajili ya soko la nyumbani Tanzania tu, mfano: UGANDA kuna Tamasha Linaitwa NYEGE FESTIVAL…. na kwa nafasi niliyonayo UGANDA na kwanjinsi nyimbo hii ilivyovuma kwa kishindo ndani ya Muda mchache tu, basi naamini kabisa Mwakani lazima NYEGE FETIVAL waniite kutumbuiza… na kama mnavyofahamu bei zangu huwaga si chini dola elf Sabini za kimarekani ( $70,000) kwa show
sawa na milioni (160,300,000 za kitanzania)…..mbazo kwa show moja tu ningeweza kuchangia pato la kodi si chini ya milioni (48,090,000 ya kitanzania)…hivyo naomba mlitazame na hapo Balaza letu Pendwa…. NNE:- Pia ikija Upande wa Kuitumbwiza stejini naomba pia mlitazame zaidi…Maana show zetu zote ni za Usiku wa manane ambapo watoto wamelala majumbani Tunaowaimbia ni Watu wazima…
na hata #WasafiFestival2018 pia ifikapo saa 12 jioni ni wenye Umri wa zaidi ya miaka 18 tu….hivyo tutaowaimbia ni watu wazima tu

TANO:- Wazee wangu wa Balaza la sanaa BASATA nilikuwa naomba Muipe sikio tena Nyimbo pale kwenye kipande cha Amber Rutty.. kwasababu Ujumbe wangu pale ni kupingana na kile kitendo, na ndiomaana nikasema “kananivuta ghetto nikapige Bunduki,… ila naogopa Centro Michezo ya Amber Rutty” …. sasa hapo ubaya wake uko sehem gani…maana naamini kupitia mstari huo utakuwa ni kama Kumbusho kwa kijana ama mtuyoyote kuwa “usidiriki kufanya, Utapelekwa jela…” sasa hapo wapi ubaya wake wazee wetu… SITA:- wazee wangu wa Basata ni siku tatu tu Tangu kutoka kwa wimbo huu, lakini kika Mwana Africa Masharikina siekuwa Mwana Africa Mashariki Apajua Nyegezi Mwanza….na naamini kulikuwa na wengi pengine hawapajui lakini kupitia wimbo ule sasa wamepajua..na naamini wengi wanatamani hata wafike akapashangae kuwa kumbe #NYEGEZI kwenyewe ndio hapa….na hio ndio miongoni mwa faida ya kazi ya sanaa wazee wetu….
Mie yangu yalikuwa hayo, na naamini Kwa Uelewa wenu na Upendo wenu mtatusaidia kwa hayo vijana wenu…Shukran
Ni mimi kijana wenu
Nasibu Abdul Juma
(Diamond Platnumz)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents