BurudaniDiamond Platnumz

Diamond kuungana na P-Square, 2 Face, Davido, Fally Ipupa, Mr Flavour kwenye tuzo za AFRIMMA 2014

Collabo na Davido imeanza kuzaa matunda kwa Diamond Platnumz. Staa huyo wa My Number One, ataungana na wasanii wakubwa wa Afrika wakiwemo na P-Square, 2 Face, Davido, Fally Ipupa, Mr Flavour, Sarkodie na wengine kwenye utoaji wa tuzo za African Muzik Magazine Awards, AFRIMMA 2014.

Tuzo hizo zimeandaliwa na Big A Entertainment na African Muzik Magazine na zitatolewa Jumamosi ya July 26, 2014 na zitajumuisha wageni kutoka Marekani na nchini 17 za Afrika. Zitashereheshwa (hosted) na mchekeshaji Basket Mouth na muigizaji wa Nollywood, Juliet Ibrahim.

“The weekend promises to be a ground breaking and revolutionary experience,” anasema mwanzilishi wa African Muzik Magazine na Big A Entertainment, Anderson Obiagwu. “It will be a night of celebrating Africa’s top artist who are influencing the music scene and culture of Africa for the better.”

Tuzo za mwaka huu zitafanyika jijini Dallas, Marekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents