BurudaniDiamond Platnumz

Diamond Platnumz atajwa kuwania tuzo za BET Awards 2014 Marekani

Baada ya kunyakua tuzo 7 za KTMA 2014, na kuwa nominated katika tuzo za MTV ‘MAMA’ nchini Afrika Kusini, sasa Diamond Platnumz ametajwa kuwania tuzo kubwa zaidi za kimataifa BET Awards za nchini Marekani.

Diamond (2)

Hit single yake ya ‘Number 1’ ndio iliyompa tiketi Diamond kuwa nominated katika kipengele cha ‘Best International Act: Africa’, ambapo anachuana na mastaa wengine wa Africa ambao ni Davido(Nigeria), Mafikizolo (Afrika Kusini), Sarkodie (Ghana), na Tiwa Savage (Nigeria).

Diamond ndiye msanii pekee wa Afrika mashariki katika tuzo hizo.

Hivi ndivyo ilivyoandikwa katika mtandao wa www.bet.com

BEST INTERNATIONAL ACT: AFRICA “NUMBER ONE” (TANZANIA)
TANZANIAN STAR DIAMOND PLATNUMZ BECAME A GLOBAL FORCE WITH SUCCESS OF HIS HIT “NUMBER ONE” AND THAT WAVE MAY CONTINUE WITH A WIN FOR BEST INTERNATIONAL ACT: AFRICA.

bet

Sherehe za ugawaji wa tuzo hizo zitafanyika June 29 huko Los Angeles, Marekani

Tuzo za BET huandaliwa na kituo cha TV cha Black Entertainment Television, na zilianzishwa mwaka 2001 kusheherekea mafanikio ya kazi za Wamarekani weusi katika sanaa ya muziki, uigizaji, michezo na maeneo mengine ya burudani.

Hongera sana Diamond Platnumz, endelea kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents