Habari

Dkt Mahiga awaonya Watanzania wanaojihusisha na ugaidi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga, amewaonya watanzania wanaoishi nje ya nchi kujitohusisha na masuala ya ugaidi ambayo yanatoa taswira mbaya kwa nchi ya Tanzania.

2

Akizungumza na wanadiaspora katika kongamano la Kitaifa la watu wanaoishi ughaibuni Dk Mahiga amesema kuwa kuna baadhi ya watanzania wameonekana kujihusisha na matukio hayo kwa tamaa zao binafsi za kifedha.

“Tatizo la kujihusisha na masuala ya kigaidi ni tishio kubwa kwa nchi ya Tanzania na ukanda mzima wa Afrika Mashariki,” alisema Dk Mahiga.

“Inagusa kuwepo kwenu uko nje, pengine mmelizungumzia hili katika mjadala wenu, nataka nizungumzie vitishio vipya vya amani na utulivu katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, moja ni tishio la ugaidi,” alisema.

“Ni tishio lenye sura tofauti tofauti, sura ya kwanza lina itikadi ya aina yake kabisa ambayo ni tofauti na imani zetu kama tunavyozielewa, sura ya pili inachukua mapambano ya kijeshi lakini mapambano ya pekee kabisa katika nchi nyingi zilizokombolewa katika ukoloni,” alifafanua.

Pia aliwakumbushia juu ya sura ya pili ya tishio la kijeshi akisema, “kipindi cha zamani watu walikuwa wanasema Guerrilla warfare, ni kwamba unashirikisha raia unapambana na adui unayemuona lakini ugaidi haushirikishi.”

BY:EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents