Burudani

Don Jazzy amwajiri mfanyakazi wa airport aliyemsaidia na kusababisha afukuzwe kazi

CEO wa Mavin Records, Don Jazzy amemwajiri mfanyakazi wa Delta Airline aliyemsaidia kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Murtala Mohammed jijini Lagos.

Mfanyakazi huyo alifukuzwa baada ya kumruhusu Don Jazzy kuendesha vigari vidogo vya uwanja wa ndege kitu ambacho ni kinyume cha sheria za uwanja wa ndege. Staa huyo aliyekuwa akielekea Durban, Afrika Kusini kuhudhuria tuzo za MTV MAMA alipost video inayomuonesha akiendesha kigari hicho wakati mfanyakazi huyo akiwa pembeni yake.,

Baadaye staa huyo alishangazwa kugundua kuwa mfanyakazi huyo alifukuzwa kazi na ndipo yeye alipoamua kumwajiri kwenye label yake.

‘Ok I took this post down before becos they threatened to fire this guy with me. Now dem don fire am. I guess I can post back since he is now my newest employee. I’m sorry bro but welcome to the Mavin Empire. u ll love it here. Osheee. (sic)’ aliandika Don Jazzy kwenye video aliyoiweka tena.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents