Burudani

Dudu Baya ataka wakuu wa Mikoa na Wilaya kusimamia uuzaji wa albamu

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Dudu Baya ameshauri kuwepo na utaratibu ambao utawahusisha Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Maafisa utamaduni katika maeneo hayo kushiriki katika kusimamia uuzaji wa albamu za wasanii ili kudhibiti wezi.


Dudu Baya kupitia E-Newz ya EATV amehoji kazi ya Afisa utamaduni katika wilaya au mkoa ni ipi zaidi ya kutoa kibali kwa wasanii wanapoenda kufanya show katika maeneo hayo na kupendekeza wafanye zaidi ya hapo.

“Serikali ina uwezo wa kuwa na duka kila mkoa kwa sababu hawa ma-distributor wa Kariakoo hawana maduka mikoani lakini sekali ina uwezo wa kumwambia Mkuu wa Mkoa kuwepo na duka katika mkoa wako na wilaya na hata Kata na nao maafisa utamaduni wakasimamie. Hapo wizi unakuta haupo, serikali inapata mapato na masanii anapata mapato,” amesema Dudu Baya.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents