Burudani

Dully Sykes awatupia lawama wasanii aliowasaidia kumtosa kwenye show yake ya miaka 15!

Dully Sykes amedai kusikitishwa na kitendo cha baadhi ya wasanii aliowataja kuwa ni ‘wadogo zake’ walioamua kumtosa kwenye show yake ya kuadhimisha miaka 15 ya muziki wake iliyofanyika jana, Escape One.

10899179_1553016814944982_1702920143_n

Akiongea na XXL ya Clouds FM, Dully amesema ameshangaa kuona kuwa wasanii wakongwe wakiwemo Mwana FA, Q-Chief, Chege, Madee, Christian Bella na wengine waliweza kumuunga mkono, lakini wasanii ‘wadogo zake’ kumchinjia baharini.

Msanii huyo mkongwe ambaye pia ni producer, amedai kuwa ni Diamond pekee ndiye aliyemuomba radhi kuwa asingeweza kuwepo kwenye show yake kwakuwa yupo ziarani nchini Rwanda.

Hata hivyo hakuweza kuwataja wasanii hao.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents