Burudani

East Coast Team kujikita kwenye filamu na biashara ya mavazi

Rapper King Crazy GK wa East Coast Team amesema baada ya soko la muziki kutofanya vizuri kwa sasa E.C.T wanajikita kwenye filamu na biashara ya nguo.

GK1

Akizungumza na XXL ya Clouds FM, GK alisema soko la muziki kwa sasa lina utata, ndio sababu ya East Coast kuamua kutumia ‘opportunity’ zingine zinazotokana na muziki ambazo ni nguo na filamu.

“Mwezi mmoja uliopita tulitengeneza East Coast t-shirt kwaajili ya kujaribu market,vipi soko unajua ,zilitengenezwa kama mia tatu hivi zimekaa kama siku nne zikawa zimeisha kwahiyo unaweza kuona demand ikoje. Kwahiyo tayari tunaandaa mikakati ya kutapika kwenye soko, kama unavyojua soko la muziki peke yake lina utata, kwahiyo lazima tutengeneze opportunity zinazotengenezwa na muziki nguo ndio moja wapo ya silaha yetu kubwa, ukiangalia katika site yetu ya East Coast utaona tumeweka sample na t-shirt moja kwa elfu 25,000 lakini zimekaa siku nne tu zikawa zimeisha kwahiyo kwakuwa demand inataka na soko ni kubwa tutatapika mavazi kama kawaida,tutapika muziki na tutapika movies hii ni sehemu ya fursa,” alisema GK.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents