Burudani

Ebitoke aweka wazi hisia zake kwa Ben Pol ‘nipo tayari kuolewa naye’

Mchekeshaji, Ebitoke kutoka Timamu African Media amefunguka kwa kudai kuwa anampenda sana muimbaji, Ben Pol.

Ebitoke amedai ameamua aweke wazi mahusiano yake kutokana na kukaa muda mrefu bila kufanya hivyo licha ya baadhi ya mashabiki kutaka kujua kuhusu mahusiano yake.

“Najua wengi hamjawahi kuona nikipost mpenzi wangu ila nimeona leo niweke wazi. Kwa muda mrefu nimeficha hisia zangu kwa mwanaume huyu sababu nilikua naogopa kumueleza ukweli leo nimeona niseme ukweli,” aliandika Ebitoke Instagram.

“Nampenda sana Ben Pol natamani awe mpenzi wangu wa maisha, sijui kama anayempenzi wake au laa ila natanguliza samahani kama nimemkosea kumueleza hisia zangu mtandaoni nahisi siwezi kumueleza live naomba mliokaribu nae mumueleze hisia zangu. Niko tayari kuolewa naye wakati wowote. Najua wengine mtanitukana au kunikejeli kua sina hadhi ya kuwa mpenzi wake.Naombeni mumfikishie ujumbe huu Ben Pol.

Mwambieni

NAMPENDA
???? ????
#TrueLove ,”  aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents