Burudani

Eminem ameigiza kwenye filamu ya ‘The Interview’ ambamo alijitangaza kuwa ni shoga (Video)

Eminem ameigiza pia kwenye filamu ya The Interview ambayo imekuwa chanzo cha kukua kwa mgogoro kati ya Marekani na Korea Kaskazini.

https://www.youtube.com/watch?v=rbWF3wMFaUQ

Kuonekana kwa Eminem kwenye filamu hiyo kunaweza kuwa kunachekesha zaidi kwa wengi pale ambapo rapper huyo anayefahamika kwa mashairi yake ya kuwaponda mashoga akimshangaza mtangazaji (nafasi iliyoigizwa na James Franco) aliposema kuwa naye ni shoga.

Kauli ya Eminem ilionekana kumwacha mdomo wazi mtangazaji huyo ambaye alionekana kutoamini alichokisikia.

Filamu ya The Interview ilisitishwa kuzinduliwa kwenye majumba ya sinema nchini Marekani siku ya Christmas baada ya hackers kutishia kufanya shambulio la kigaidi kama lile la September 11.

Badala yake kampuni ya Sony iliamua kuizindua filamu hiyo mtandaoni na hadi sasa imeshaingiza zaidi ya dola milioni 15 na kufanya kuwa filamu ya kampuni hiyo iliyowahi kupakuliwa zaidi mtandaoni.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents